Tovuti ya OnIslam imeripoti kuwa, kongamano hilo litasimamiwa na kitengo cha teolojia cha Chuo Kikuu cha Howard kwa lengo la kuzidisha mazungumzo na kuhamasisha mijadala ya kubadilishana mawazo kati ya wanachuo, viongozi wa jamii na wanafunzi wa taaluma za sayansi ya Qur'ani na tafsiri ya kitabu hicho.
Kongamano hilo litajadili utafiti wa masuala ya Qur'ani kuanzia muundo wa kitabu hicho na maana ya aza zake na mbinu mpya za kiraa ya Qur'ani kwa kutilia maanani changamoto za kidini, kimaadili na kijamii.
Masuala mengine yatakayojadiliwa ni msimamo wa Qur'ani kuhusu Mayahudi na Wakristo, maadili ya Qur'ani, jinsia katika Qur'ani, utafiti wa masuala ya Qur'ani na mjadala juu ya sura za kitabu hicho. 1096760