Katika ujumbe wake kupitia mtandao wa kijamii X, shirika hilo lilieleza: “Katika Gaza, kinachohitajika tu ili kuzuia njaa hii ya kutengenezwa ni nia ya kisiasa na kuondoa marufuku dhidi ya misaada ya UNRWA.”
Taarifa ya Integrated Food Security Phase Classification (IPC) ya tarehe 22 Agosti ilibainisha kuwa njaa kali imekita mizizi kaskazini mwa Gaza, na ikatoa tahadhari kuwa hali hiyo inaweza kuenea zaidi endapo mzingiro wa Israel utaendelea. Utawala wa Kiayuni wa Israel unatumia njaa kama silaha ya vita dhidi ya Israel.
Kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Gaza, watu 387 wakiwemo watoto 138, wamefariki kutokana na utapiamlo mkali na njaa tangu Oktoba 2023.
UNRWA imekuwa ikitoa wito wa kusitisha mapigano kwa zaidi ya siku 700, na imesisitiza tena wito huo:
“Misaada yetu ya kibinadamu, iliyopigwa marufuku na mamlaka ya Israeli—ingeweza kuokoa maisha.”
Tangu Oktoba 2023, kampeni ya kijeshi ya mauaji ya kimbari ya utawala wa Israel imewaua zaidi ya Wapalestina 64,000 katika mashambulizi makali yaliyoisambaratisha Gaza.
Mnamo Novemba mwaka jana, Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) ilitoa hati za kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu na aliyekuwa waziri wa vita Yoav Gallant kwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu huko Gaza.
Aidha, Israeli inakabiliwa na kesi ya mauaji ya halaiki (genocide) katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kutokana na vita vyake dhidi ya eneo hilo.
3494532