Akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano wa 39 wa Kimataifa wa Umoja wa Kiislamu uliofanyika Tehran siku ya Jumatatu, Mufti Hasanović alisisitiza kuwa Mtume Muhammad (SAW) alikuwa mfano wa rehema, ambaye wanadamu wote na viumbe vyote walinufaika naye.
“Ummah unapaswa kuwa kioo cha rehema katika nyanja zote; hivyo ni lazima tueneze rehema ili tuione ikidhihirika katika maisha yetu yote,” alieleza.
Mufti Mkuu huyo aliongeza:
“Leo hatuwezi kuzungumzia rehema wakati jinai za utawala wa Kizayuni zinaendelea huko Gaza. Mandhari ya Gaza ni mtihani mkubwa wa kimungu. Kila kona ya Gaza tunasikia vilio vya watoto na wanawake.”
Alihoji:
“Je, kwa hakika tunadhihirisha rehema ya Uislamu leo? Ni lazima tuitekeleze rehema ya zama za Mtume (SAW) katika matendo yetu.”
Sheikh Hasanović alisisitiza kuwa Ummah wa Kiislamu una jukumu la kuiga mwenendo na tabia ya Mtume (SAW) na kuandaa mazingira yatakayowawezesha Waislamu wote kuifuata njia hiyo.
“Wanazuoni wote wa Kiislamu wanapaswa kutekeleza majukumu yao na kuwasaidia Wapalestina—si kwa maneno tu bali kwa vitendo. Ni lazima tuwasaidie na kuwa mashujaa wa haki yao,” alihitimisha.
Ammar al-Hakim, kiongozi wa Harakati ya Hekima ya Kitaifa ya Iraq, pia alihutubia mkutano huo. Alisema:
“Umoja haumaanishi kuacha imani zetu, bali ni kuungana dhidi ya changamoto zinazolenga uwepo wetu katika ngazi ya kimataifa.”
Al-Hakim alieleza kuwa jamii ya Iraq imeungana na kufungua mikono yake kwa Ummah wa Kiislamu. Akiashiria vita ya siku 12 iliyolazimishwa na Israel dhidi ya ardhi ya Iran, alisisitiza kuwa:
“Umoja, mshikamano, na uratibu kati ya wananchi na uongozi wa Iran vilikuwa miongoni mwa nguzo muhimu za nguvu zilizolinda nchi hiyo dhidi ya mashambulizi ya Israeli.”
Alionya kuhusu mpango wa utawala wa Kizayuni wa “Israeli Kubwa” na akasema kuwa Israel inalenga kupanua mipaka yake kwa kuvamia ardhi za Waislamu, jambo ambalo ni changamoto kubwa kwa ulimwengu wa Kiislamu na mataifa yote ya eneo hilo.
“Kujisalimisha kwa Israel kutasababisha mataifa ya Kiislamu kushindwa mara kwa mara,” aliongeza.
3494524