Rais Mahmoud Ahmadinejad amesema hayo alipokutana na Antonio Guterres, Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) hapa mjini Tehran.
Ameongeza kwamba, kuwashughulikia wakimbizi ni suala la kibinadamu na watu wote duniani wanaelewa kwamba wana jukumu la kuwasaidia wakimbizi katika sehemu yoyote duniani.
Rais Ahmadinejad amesema ana matumiani kuwa kwa msaada na ushirikiano wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) mfumo wa kusimamia masuala ya dunia ufatafanyiwa marekebisho, uadilifu utaenea duniani na wakimbizi wote watarejea katika nchi zao.
Kwa upande wake Antonio Guterres Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) ameishukuru Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kuwapa hifadhi wakimbizi wa Kiafghani na kusema kwamba, suala hilo linaonyesha ukarimu wa taifa la Iran.
Guterres pia amebainisha kwamba shirika la UNHCR halijafanya chochote ikilinganishwa na msaada uliotolewa na Iran kwa wakimbizi. 1099141