Sayyid Hassan aliyeyasema hayo katikati ya mamilioni ya waandamanaji mjini Beirut, Lebanon ameziambia nchi za Kiislamu zinazozembea kupitisha sheria ya kutambua kuvunjiwa heshima matukufu ya dini za mbinguni kuwa, ni kuzembea kujua haki ya mtukufu Mtume Muhammad SAW Amesema kuwa, viongozi wa Marekani lazima wajue kuwa, kuruhusu kujengwa na kusambazwa kwa filamu iliyoyavunjia heshima matukufu ya Kiislamu, ni hatari zaidi kwa nchi hiyo ya kibeberu. Katibu Mkuu huyo wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon aliyeshiriki katika maandamano hayo makubwa ya kulaani ubaguzi wa kidini kwa kumvunjia heshima Mtume wa Uislamu, alitoa hutuba fupi na kuwataka waandamani hao kuitikia wito wa mtukufu Mtume Muhammad SAW. Amesisitiza kuwa, ulimwengu wa Kiislamu lazima utambue kwamba, Waislamu watasimama kidete dhidi ya njama za kuyavunjia heshima matukufu ya Kiislamu na Mtume wao na kwamba, anasikitishwa kuwaona baadhi ya watu wakidai kuwa filamu hiyo haijafikia kiwango cha kumtusi Mtume wa Uislamu, katika hali ambayo video ya filamu hiyo inauvunjia heshima Uislamu, Mtukufu Mtume Muhammad SAW na maisha yake na Qur'ani tukufu. Katika upande mwingine Sayyid Hassan Nasrullah pia ameutaka Umoja wa Mataifa kupitisha azimio linalopinga kuvunjiwa matukufu ya dini za Mwenyezi Mungu.
1101024