Raja Pervez Ashraf Waziri Mkuu wa Pakistan ameiamuru Wizara ya Habari ya nchi hiyo kuufunga ukurasa wa You Tube na hivyo kuzuia kutazamwa filamu hiyo dhidi ya Mtume Muhammad (s.a.w).
Waziri Mkuu wa Pakistan ameamuru kuzuiwa kutazamwa kwa filamu hiyo chafu baada ya ukurasa wa You Tube kukataa ushauri wa serikali ya Pakistan iliyotaka kuondolewa kwa filamu hiyo katika ukurasa huo.
Wakati huo huo maelfu ya Waislamu wamefanya maandamano makubwa mbele ya ubalozi mdogo wa Marekani mjini Karachi na kulaani filamu ya Kimarekani inayomvunjia heshima Mtume (saw). 1101141