IQNA

Waislamu waandamana kulaani kuvujiwa heshima Mtume SAW

14:05 - September 22, 2012
Habari ID: 2416280
Maandamano ya kupinga filamu ya Kimarekani na vijikatuni vya Kifaransa vinavyomvunjia heshima Mtume Muhammad (saw) yameendelea kufanyika katika nchi mbalimbali duniani.
Maandamano hayo yaliyofanyika baada ya sala za Ijumaa ya yameshuhudiwa nje ya balozi za Ufaransa na Marekani katika miji mbali mbali ya Misri, Lebanon, Pakistan, Yemen, Libya, Tunisia, Indonesia, Bangladesh, Saudi Arabia na hata katika nchi zisizo za Kiislamu kama vile Ujerumani. Miji ya Iran pia imeshuhudia maandamano makubwa ya kulaani vitendo vya kumvujia heshima Mtume SAW. Walindamana waliliga nara za "mauti kwa Marekani", "mauti kwa Israel" "mauti kwa Ufaransa" na "mauati kwa Uingereza".

Aidha katika maandamano hayo kote duniani, Waislamu wametangaza mahaba yao kwa Mtume wa rehma Mohammad SAW na kusema wako tayari kujitolea mhanga kwa ajili ya kumtetea.
Ikumbukwe kuwa huku ulimwengu wa Kiislamu ukiwa katika ghadhabu kufuatia hatua ya kutengenezwa filamu inayomvunjia heshima Mtume SAW huko Marekani na hivyo kuumiza hisia za Waislamu, jarida moja la Ufaransa limethubutu kuvunjia heshima matukufu wa Kiislamu.
Katika hatua ya kindumakuwili serikali ya Ufaransa imelifunga na kulipokonya leseni jarida moja nchini humo ambalo limechapisha picha za tupu za familia ya mke wa mrithi wa kiti cha ufalme wa Uingereza. Hii ni katika hali ambayo majarida ambayo yanayavunjia heshima matukufu ya Kiislamu nchini humo yameachwa kuendeleza shughuli zao bali hata yanahimizwa kuendeleza ushenzi dhidi ya Waislamu na Uislamu.
captcha