IQNA

Waislamu Marekani waandamana kupinga filamu inayomvunjia heshima Mtume (saw

22:58 - September 22, 2012
Habari ID: 2417209
Mamia ya Waislamu wa Marekani wameandamana katika mji wa Dearborn katika jimbo la Michigan wakipinga filamu na vibonzo vinavyomvunjia heshima Mtume Muhammad (saw).
Maandamano hayo yameitishwa na Kituo cha Kiislamu cha Marekani kwa lengo la kukabiliana na chuki na kueneza amani, nia njema na urafiki.
Maafisa wa Kituo cha Kiislamu cha Marekani wametangaza kuwa malengo mengine ya maandamano hayo ni kutoa mafunzo kuhusu Uislamu na utamaduni wa nchi za Waislamu.
Alkhamisi iliyopita pia viongozi wa dini mbalimbali na viongozi wa serikali wa eneo hilo walifanya maandamano mbele ya ofisi za Kituo cha Kiislamu wakipinga vitendo vya kumvunjia heshima Mtume wa Mwenyezi Mungu.
Waandamanaji hao walishikana mikono kama ishara ya umoja na mshikamano na kutangaza upinzani wao dhidi ya juhudi zinazofanywa kwa ajili ya kueneza chuki na uhasama wa kidini. 1104207
captcha