Waziri wa Reli wa Pakistan Ghulam Ahmad Bilor amewaambia waandishi habari kwamba atampa zawadi ya dola laki moja mtu yeyote atakayemuua mtayarishaji wa filamu ya Innocence of Muslims.
Amesema: Nikimpata mtu huyo aliyetengeneza filamu inayomdhalilisha Mtume (saw) nitamuua mimi mwenyewe na baadaye nitakuwa tayari kunyongwa.
Maandamano ya kupinga filamu inayomvunjia heshima Mtume Muhammad (saw) yanaendelea kufanyika katika nchi mbalimbali duniani. 1104628