Waislamu hao waliokuwa wakipiga nara dhidi ya Marekani waliandamana hapo jana na kutoa tamko dhidi ya wanaoshambulia na kuudhalilisha Uislamu.
Akitoa tamko la Waislamu mwishoni mwa maandamano hayo, Sheikh Ponda Issa Ponda, Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, ameitaka serikali ya Tanzania kuzuia mitandao ya intaneti, DVD na mianya mingine kuonyesha filamu hiyo ya kumvunjia heshima Mtume, sambamba na kutaka kufungwa ubalozi wa Marekani nchini humo.
Aidha Sheikh Ponda Issa Ponda amesema kuwa, tamko hilo ni la Waislamu wote wanaompigania Mtume na kwamba, kuanzia sasa Waislamu wanagomea bidhaa zote zinazotengenezwa na Marekani pamoja na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Ameongeza kwamba, ubalozi wa Marekani nchini Tanzania unapaswa kufungwa mara moja, la sivyo Waislamu wa nchi hiyo watachukua hatua kali zaidi.
1104893