Katika wiki hii kunatekelezwa ratiba iliyopewa jina la "Sala Milioni Moja kwa ajili ya Mtume wa Mwenyezi Mungu" katika maeneo yote ya mkoa wa Bahrul Ahmar.
Miongoni mwa ratiba za wiki hii ni vikao vya kidini katika misikiti, shule na majumba ya sinema yanayoonesha filamu zinazohusiana na sira ya Mtume (saw).
Lengo la wiki hiyo ni kuwaelewesha watu wa eneo hilo kiwango cha njama zinazofanywa dhidi ya Uislamu na kuwataka wananchi walinde umoja na mshikamano kwa shabaha ya kukabiliana na njama hizo. 1106527