IQNA

Misikiti mingi ya Algeria haikuelekea kibla

17:46 - September 25, 2012
Habari ID: 2419701
Mtaalamu mmoja wa masuala ya kidini wa Algeria amesema kuwa asilimia 80 watu wa nchi hiyo wanaelekea kusikokuwa kibla wakati wa swala.
Laabidi Milyani ambaye ni mtaalamu wa kuainisha upande wa kibla amesema kuwa, misikiti mingi ya Algeria haikuelekezwa kibla wakati wa kujengwa na kwamba watu wanaotekeleza ibada ya swala wanaelekea Baitul Muqaddas na hata Yemen wakati wanapotekeleza ibada hiyo.
Amesema kuwa baada ya kufanya uchunguzi amegundua kuwa baadhi ya misikiti hiyo imeelekezwa Vatican na kwamba msikiti Mkuu wa Algeria umeelekezwa Somalia.
Mtaalamu huyo amesema kuwa hakuna matarajio ya kuvunjwa misikiti hiyo lakini watu wanaoteleza swala ndani yake wanapaswa kuambia upande sahihi wa kibla.
Katika siku za huko nyuma kulizungumziwa suala kwamba baadhi ya misikiti ya Makka pia haikuelekea kibla, jambo ambalo lilizusha mjadala mkubwa kati ya Waislamu. 1106867

captcha