Magaidi hao pia wamemjeruhi mkuu wa kitengo cha kanali hiyo cha mjini Damascus Hussein Murtadha.
Naser alishambuliwa alipokuwa akiripoti moja kwa moja kwa kulengwa na mtu aliymkusudia kutoka mbali. Wawili hao walikuwa wakituma habari kuhusiana na milipuko iliyotekea hivi karibuni mjini Damascus.
Mkurugenzi wa Habari wa Kanali ya Press TV Hamid Reza Emadi amesema kuwa, nchi za Uturuki, Saudi Arabia na Qatar ambazo zinawapa silaha wanamgambo wa Syria ili kuua raia, askari jeshi na waandishi habari ndio zinabeba jukumu la mauaji hayo. Amesisitiza kwamba, kanali ya Televisheni ya Press TV itafuatilia mauaji hayo ya Maya na kwamba wale waliomuua ripota huyo wasifikiri kwamba wanaweza kuua waandishi habari bila kufanya lolote.
Maya Naser alizaliwa mwaka 1979 na kusoma Elimu ya Siasa katika chuo kikuu cha Marekani cha KUPLAN, alikuwa anazijua vyema lugha za Kiarabu na Kiingereza na alifanya kazi katika nchi nyingi ikiwemo Marekani, Syria, Lebanon, Jordan Misri na Bahrain. 1108036