IQNA

Filamu ya al Widaa kutengenezwa kujibu filamu inayomdhalilisha Mtume (saw)

13:59 - September 29, 2012
Habari ID: 2421898
Ahmad Ismail al-Hariri, mtengeneza filamu wa Misri amesema kuwa hatua za mwanzoni za kutengeneza filamu ya al-Widaa ambayo itajibu filamu iliyotenegenezwa na Wamarekani pamoja na Wazayuni kwa lengo la kumdhalilisha mtume Mtukufu wa Uislamu (saw) zimekamilika.
Amesema filamu hiyo itazungumzia maisha ya Mtume miaka mitano kabla ya kuaga kwake dunia na kwamba thuluthi moja ya filamu hiyo itaangazia siku ya kifo chake.
Al-Hariri amesema amechukua uamuzi wa kutenegeneza filamu hiyo ili kujibu filamu iliyotenegenezwa na Wamarekani na Wazayuni kwa lengo la kumdhalilisha Mtume Mtukufu (saw).
Amesema filamu hiyo ambayo haitakuwa ya nara tu italenga kujibu upotofu uliotegemewa na waovu na maadui wa Kiislamu kumdhalilisha Mtume (saw). 1108796
captcha