Kwa mujibu wa tovuti ya aps, utafiti huo uliofanywa na Chuo Kikuu cha Swansea nchini Uingereza unaonyesha kwamba, mwaka 2011 karibu Waingereza 5200 walisilimu ambapo asilimia 75 ya Waislamu hao wapya ni wanawake.
Uchunguzi huo pia unathibitisha kwamba katika kipindi cha miaka 10 iliyopita karibu Waingereza laki moja wameukubali Uislamu na kusilimu ambapo robo tatu ya hao ni wanawake.
Utafiti huo pia umeashiria matatizo malimbali yanayowakabili Waislamu wa Uingereza na kusema kuwa, chanzo cha matatizo hayo hutokana na familia zao ambazo huwa na mtazamo mbaya na usiozingatia ukweli kuhusiana na dini hii tukufu.
Tatizo jingine la Waislamu hao wapya ni kuwa hawana chombo kimoja maalumu kinachoweza kushughulikia matatizo yao na kuwaongoza kwenye njia nyoofu. Suala hilo huyaachia fursa makundi tofauti ya Kiislamu yaliyo na itikadi zinazogongana kuwachanganya zaidi Waislamu hao wapya. 1109058