IQNA

Maonyesho ya kaligrafia ya aya za Qur'ani yafanyika Palestina

16:01 - September 30, 2012
Habari ID: 2423068
Said an-Nahri, msanii na mwanakaligrafia mashuhuri wa Palestina ameandaa maonyesho maalumu katika mji wa Sakhnain kaskazini mwa Palestina ambapo ameonyesha makumi ya loho mbalimbali zilizopambwa kwa hadithi za Mtume (saw) na aya za Qur'ani zilizoandikwa kwa mbinu maalumu za kaligrafia.
Mbinu za kaligrafia zilizotumiwa na msanii huyo ni za aina yake kwa kuwa ametegemea sana mazingira ya kawaida katika uandishi huo. Anaamini kwamba mbinu hiyo ina nafasi muhimu katika kulinda aya, thamani za sanaa na historia ya Kiislamu.
An-Nahri anasema Qur'ani Tukufu ni maandishi yenye thamani kubwa zaidi kati ya maandishi yote ya Kiarabu na kwamba katika kazi zake zote amejaribu kuonyesha mapambo ya aya za Qur'ani pembeni ya maana halisi ya aya hizo.
Hadi sasa amechora na kuandika maandishi tofauti ya kaligrafia katika loho 400 na kuuza baadhi yazo kwa bei nafuu. 1110269
captcha