IQNA

Washindi wa mashindano ya utafiti wa Qur'ani watangazwa Iraq

18:16 - October 01, 2012
Habari ID: 2423863
Watu watano walioshinda katika mashindano ya utafiti bora wa Qur'ani wamearifishwa katika shughuli iliyosimamiwa na Kituo cha Taifa cha Sayansi za Qur'ani na Turathi za Kiraa nchini Iraq.
Mkurugenzi wa kituo hicho Adel al Kinani amesema kuwa tafiti tano zimeteuliwa kwa kuzingatia vigezo makini vya kielimu na kwamba utafiti wa Ali Zein umeshika nafasi ya kwanza.
Mkurugenzi w Kituo cha Kitaifa cha Sayansi za Qur'ani cha Iraq amesema kuwa shughuli za Wiki ya Nne ya Qur'ani nchini humo zingali zinaendelea katika sehemu kadhaa kama mashindano ya Qur'ani, hifdhi na tafsiri ya kitabu hicho kitukufu. 1111067
captcha