IQNA

OIC yaitaka UN kutekeleza maazimio yanayopiga marufuku kuvunjiwa heshima matukufu ya kidini

18:44 - October 01, 2012
Habari ID: 2423868
Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imelitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutekeleza maazimio yanayopiga marufuku kuvunjiwa heshima matukufu ya kidini.
Katibu Mkuu wa OIC Ekmeleddin Ihsanoglu ameashiria maazimio hayo ya Umoja wa Mataifa na kusema kuwa sheria hizo zinapaswa kutekelezwa.
Amesema kuwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na Baraza la Haki za Binadamu yalipasisha sheria zinazopiga marufuku kuvunjiwa heshima matukufu ya kidini.
Ihsanoglu amesema hayo siku kadhaa baada ya mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za Kiislamu kutoa taarifa wakilaani filamu ya Kimarekani inayomvunjia heshima Mtume Muhammad (saw).
Taarifa hiyo ilisema kuwa filamu hiyo inachochea uhasama, ubaguzi na uadui dhidi ya Waislamu, dini ya amani ya Uislamu na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw). 1111314
captcha