Kwa mujibu wa makala iliyoandikwa na Kevin Barret katika safu ya makala za kisiasa ya mtandao wa televisheni ya Press TV, si mwiko tena sasa kusikia afisa rasmi wa Marekani akiungama waziwazi kwamba suala la kuporomoka kwa Israel ni jambo lisiloweza kuzuilika.
Kwa mujibu wa Barret, ripoti ya utafiti uliofanywa mapema mwaka huu na Jumuiya ya Mashirika ya Kiintelijinsia ya Marekani inayojumuisha mashirika 16 ya nchi hiyo chini ya anuani isemayo" Kujiandaa kwa Mashariki ya Kati ya baada ya Israel" nayo pia imethibitisha na kutilia nguvu maelezo ya Kissinger ambaye yeye mwenyewe pia ni Myahudi.
Mchambuzi huyo wa masuala ya kisiasa amesema ripoti hiyo imesisitiza kwamba serikali ya Marekani haina uwezo tena wa kijeshi na kifedha wa kuisaidia Israel kukabiliana na matakwa ya zaidi ya watu bilioni moja katika nchi zilizo jirani yake na kushauri kuwa Washington itapaswa kufikiria maslahi yake ya kitaifa na kuuacha mkono utawala huo wa Kizayuni.
Kwa mujibu wa Kevin Barret kuna sababu kadhaa ambazo zimepelekea kujitokeza kwa hali hiyo ikiwemo kuchoshwa wanasiasa na wanaharakati wa kisiasa wa Marekani na sera za kufurutu mpaka za Israel na kutokuwepo tena umoja ndani ya jamii ya Kiyahudi ya Marekani katika suala la kuunga mkono utawala huo wa Kizayuni.