Hazeti la al Masri al Youm limeripoti kuwa, Majdi al Gheiti ambaye alikuwa mshindani Mskristo katika mashindano hayo amefanikiwa kushika nafasi ya pili. Mkristo huyo amechuana na washiriki wengine 19 ambao wote walikuwa Waislamu.
Al Gheiti amesema kuwa katika mashindano hayo ya maandishi ametumia masaa manne kujibu maswali 20 yanayohusiana na Qur'ani na kushika nafasi ya pili.
Majdi al Gheiti amesema kuwa lengo la kushiriki katika mashindano hayo ya Qur'ani ni kuonesha udugu na umoja kati ya Waislamu na Wakristo nchini Misri na kulidhihirisha eneo la al Muusara kuwa nembo na kigezo bora cha kuisha kwa amani kati ya raia Wakristo na wenzao Waislamu. 1111681