Sheikh Yahya al-Halili, MuhamMad Jam'an na Swadiq Abdallah wamesimamia visomo vya makarii 33 wa kitaifa ambao walisoma Qur'an kwa visomo tofauti.
Fuad ar-Ruhani, mmoja wa wasimamizi wa mashindano hayo amesema kuwa makarii 50 wa Yemen wameshiriki katika mashindano hayo ambayo yamepangwa kumalizika leo Jumatano.
Washindi wa mashindano hayo pamoja na wengine walioshiriki katika mashindano ya miaka ya 2010 na 2011 wanatazamiwa kupewa zawadi zao katika sherehe maalumu ambayo imepangwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu. 1112621