Idara ya Wakfu ya Mashia ndiyo iliyoandaa marasimu hayo yaliyofanyika katika mji mtakatifu wa Karbala. Marasimu hayo yalifanyika siku ya Jumatatu ikiwa ni moja ya shughuli za wiki ya nne ya ratiba ya kila mwaka ya kufarijika na Qur'ani Tukufu.
Akizungumza katika marasimu hayo, Adil al-Kanani mkuu wa Kituo cha Kitaifa cha Masomo ya Qur'ani na Turathi ya Kiraa kinachofungamana na Idara ya Wakfu ya Mashia wa Iraq amesema kuwa, kujipamba kwa sifa nzuri za Qur'ani ni moja ya njia bora zaidi za kukabiliana na waovu wa Magharibi wanaomvunjia heshima Mtume (saw) pamoja na Qur'ani Tukufu. Amesema Waislamu wanapasa kutumia njia zote za amani kusahihisha fikra potofu iliyoenezwa duniani na maadui wa Kiislamu kuhusiana na mafundisho ya dini hii tukufu.
Mzungumzaji mwingine katika marasimu hayo alikuwa Hamid al-Mukhtar, mkuu wa masuala ya kiutamaduni katika ofisi ya Shahid Sadr ambaye alisisitiza udharura wa kuzingatiwa mafundisho ya Qur'ani na wahubiri wa kitabu hicho kitakatifu pamoja na kutotumbukia katika mtego wa maadui wa wa kutaka kuwagonganisha wafuasi wa dini tofauti za mbinguni. 1112795