IQNA

Mjumbe wa Katibu Mkuu wa UN kukutana na Sayyid Nasrullah

16:32 - October 03, 2012
Habari ID: 2425454
Mjumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Syria anatarajiwa kukutana na kiongozi wa Hizbullah ya Lebanon Sayyid Hassan Nasrullah.
Lakhdar Brahimi anatazamiwa kuzitembelea Saudia na Lebanon na kukutana na viongozi wa ngazi za juu wa nchi hizo katika siku chache zijazo.
Miongoni mwa ajenda za safari ya Brahimi nchini Lebanon ni kukutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Hizbullah Hassan Nasrullah na pande hizo mbili zitajadili mgogoro wa Syria.
Kabla ya safari hiyo Brahimi amefanya safari nchini Syria na kukutana na viongozi wa makundi mbalimbali ya nchi hiyo. Vilevile alikutana na kufanya mazungumzo na Rais Bashar Assad na viongozi wa kambi ya upinzani. 1113071
captcha