IQNA

Mashindano ya kitaifa ya Qur’ani yaanza Yemen

22:10 - October 03, 2012
Habari ID: 2425489
Mashindano ya 14 ya Kitaifa ya Qur’ani nchini Yemen yameanza Oktoba pili katika mji mkuu Sana’a.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mashindano hayo yanafanyika kwa lengo la kuwakurubisha zaidi vijana na mafundisho ya Qur’ani Tukufu.
Jopo la majaji katika mashindano hayo ni wataalamu wa Qur’ani kutoka huko huko Yemeni. Mashindano hayo ya siku mbili yana washiriki 50 ambao watatunukiwa zawadi za kifedha wakati wa sherehe za kuyafunga.
Pembizoni mwa mashindano hayo kuna shindano kuhusu ubunifu wa Kisayansi wa vijana kuhusu Sayansi za Qur’ani.
1112621


captcha