IQNA

Ayatullah Khatami:

Marekani imeanzisha vita kamili vya kiuchumi dhidi ya Iran

5:46 - October 06, 2012
Habari ID: 2426129
Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa mjini Tehran amelaani vikali hatua ya Marekani ya kuliondoa kundi la kigaidi la MKO katika orodha yake ya makundi ya kigaidi.
Ayatullah Ahmad Khatami amesema hayo katika hadhara ya waumini waliohudhuria ibada ya kisiasa na kimaanawi ya Sala ya Ijumaa na kubainisha kwamba, baadhi ya jinai na mauaji ya kundi la kigaidi la Munafiqina MKO yalifanywa kwa amri ya Marekani.
Sayyid Khatami ameashiria jinai za MKO na kubainisha kwamba, wananchi wengi wa Iran wakiwemo shakhsia muhimu waliuawa shahidi katika matukio mbalimbali ya jinai za kundi hilo la kigaidi.
Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya Tehran amesema kwamba, katika hali ya hivi sasa haiwezekani kufanya mazungumzo na Marekani. Ayatullah Khatami ameashiria mashinikizo ya madola ya kibeberu dhidi ya Iran na kubainisha kwamba, mashinikizo hayo ni vita kamili vya kiuchumi.
Ameongeza kwamba, kama ambavyo madola ya Magharibi hayakufikia malengo yao katika vita vya miaka minane vilivyoanzishwa na dikteta Saddam dhidi ya Iran, leo hii pia hayatoweza kulifanya taifa la Iran liyapigie magoti. 1113632
captcha