IQNA

Kazakhstan yapiga marufuku filamu ya Marekani inayotusi Uislamu

21:27 - October 06, 2012
Habari ID: 2426441
Mahakama moja nchini Kazakhstan imepiga marufuku filamu ya Marekani inayomvunjia heshima Mtume Mtukufu (saw).
Kwa mujibu wa tovuti ya lefigaro, mahakama hiyo imesema kuwa imechukua hatua hiyo baada ya kuchunguza kwa makini filamu hiyo na kuamua kuwa ni nembo ya dharau na upindukiaji mipaka dhidi ya matukufu ya Kiislamu.
Mahakama hiyo ya mjini Astara mji mkuu wa Kazakhstan, imeongeza kuwa baada ya kuona kuwa filamu hiyo inatusi na kuvunjia heshima matukufu ya Kiislamu, imeamua kuipiga marufuku na kwamba hakuna mtu yoyote anayepasa kuonyesha, kukopi, kusambaza, au kutumia sehemu zake katika utengenezaji wa filamu nyingine.
Sababu nyingine iliyotegemewa na mahakama hiyo kupiga marufuku filamu hiyo ni kwamba inaeneza chuki ya kidini dhidi ya Waislamu.
Kabla ya hapo nchi nyingine za Kiislamu na zisizo za Kiislamu kama vile Iran, Saudi Arabia, Uturuki, Lebanon, Misri, Tunisia na Russia zilipiga marufuku filamu hiyo kwa sababu zinazofanana na hizo. 1113570
captcha