IQNA

Hizbullah ya Lebanon yalaani jinai za Israel katika Msikiti wa al-Aqsa

21:36 - October 06, 2012
Habari ID: 2426443
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Lebanon Hizbullah imetoa taarifa ikilaani vikali jinai za hivi karibuni za utawala haramu wa Israel dhidi ya matukufu ya Kikristo na Kiislamu katika msikiti mtukufu wa al-Aqsa.
Kwa mujibu wa tovuti ya al-Manar, Hizbullah imesema katika taarifa hiyo kwamba kila siku walowezi wa Kizayuni katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina hutekeleza jinai mpya dhidi ya matukufu ya Wakristo na Waislamu. Imesema jinai ya hivi karibuni ni hujuma kubwa iliyofanywa na walowezi hao wakisaidiwa na polisi ya Israel kwa lengo la kuteka uwanja wa Msikiti wa al-Aqsa na kuwachochea waumini waliokuwa wakiswali humo.
Hizbullah imeyataka mataifa ya Kiarabu na Kiislamu katika taarifa hiyo kuunga mkono na kutetea matukufu ya kidini katika msikiti huo.
Jumuiya za kimataifa pia zimetakiwa kutekeleza majukumu yao kuhusiana na taifa linalodhulumiwa la Palestina na vilevile kutetea matukufu ya Waislamu na Wakristo katika eneo la msikiti huo. 1113575
captcha