IQNA

Uandikishaji majina wa washiriki wa mashindano ya Qur'ani ya Imarati waanza

21:43 - October 06, 2012
Habari ID: 2426445
Taasisi ya Qur'ani na Suna ya Sharjah katika Umoja wa Falme za Kiarabu imetangaza kuwa imeanza kusajili majina ya watu watakaoshiriki katika duru ya 16 ya mashindano ya hifdhi ya Qur'ani na Hadithi za Mtume (saw).
Kwa mujibu wa shirika rasmi la habari la Imarati WAM, wanawake na wanaume walio na umri tofauti wanaweza kushiriki katika mashindano hayo na tayari kamati maalumu zimeundwa kwa lengo la kutoa maelezo kuhusiana na masuala tofauti ya mashindano hayo.
Kamati ya habari na maelezo tayari imeweka mabango ya matangazo ya mashindano hayo katika sehemu mbalimbali za mji wa Sharjah.
Kuwashajiisha vijana wahifadhi Qur'ani na kujifunza tajwidi ni miongoni mwa malengo ya kufanyika mashindano hayo.
Tayari duru 15 za mashindano hayo zimeshafanyika ambapo washindi walio na umri tofauti wametunukiwa zawadi maalumu. Usajili wa majina ya washindani walio na hamu ya kushiriki katika mashindano hayo utaendelea hadi tarehe 18 Oktoba na taasisi mbalimbali za Qur'ani zimealikwa kuwasilisha majina ya wawakilishi wao katika makundi tofauti ya mashindano hayo.
Hatua ya kwanza ya hifdhi ya Qur'ani imepangwa kufanyika tarehe 24 Novemba na ya hifdhi ya Hadithi za Mtume tarehe 25 Januari katika majengo mapya ya Taasisi ya Qur'ani na Suna mjini Sharjah. 1113645
captcha