Waziri wa Wakfu wa serikali iliyochaguliwa na wananchi wa Palestina Ismail Ridhwan amesema wizara hiyo itaitisha mashindano ya kimataifa ya Qur'ani yalipewa jina la Quds ambayo yatawashirikisha washindani kutoka nchi mbalimbali duniani.
Ismail Ridhwan amesema kuwa, mashindano hayo yatafanyika kwa lengo la kuvunja mzingiro wa Wazayuni dhidi ya Ukanda wa Gaza ambao unaendelea kwa kipindi cha miaka sita sasa.
Waziri wa Wakfu wa Palestina amesema kuwa lengo jingine la mashindano hayo ni kuimarisha mshikamano wa umma wa Kiislamu na Quds Tukufu ambayo imekuwa ikikabiliwa na mashambulizi ya kila siku ya utawala ghasibu wa Israel.
Washindi wa mashindano hayo ya kimataifa ya Qur'ani watatunukiwa zawadi katika sherehe itakayofanyika mwezi Ramadhani mwaka 1434 Hijria.
1115429