Tovuti ya Mooslym imeripoti kuwa, uamuzi wa kusimamishwa uuzaji wa mchezo huo wa kompyuta umechukuliwa baada ya malalamiko ya Waislamu wanaosema kuwa mchezo huo unavunjia heshima matukufu ya dini yao.
Mchezo huo uliopewa jina la "Call Of Duty Modern Warfare 2" unatumia hadithi za Mtume Muhammad (saw) katika maeneo yasiyofaa, suala ambalo ni aina fulamu ya kuvunjia heshima na kukejeli matukufu ya Waislamu.
Mmoja wa maafisa wa kampuni hiyo amewaomba radhi Waislamu kutokana na makosa hayo na kusema kuwa kitendo hicho hakikufanyika kwa makusidi na kwamba hawakuwa na nia ya kuwavunjia heshima Waislamu.
Afisa huyo ameahidi kuondoa vipengee vyote visivyofaa katika mchezo huo na kuwa makini zaidi katika kazi nyingine za kampuni hiyo.
Kampuni ya Activision imesema kampuni hiyo na washirika wake wanaheshimu dini na tamaduni mbalimbali na wanajali malalamiko ya wateja wao.
Hii si mara ya kwanza kwa michezo ya kompyuta inayotengenezwa Marekani na nchi nyingine kuvunjia heshima matukufu ya Kiislamu. Mwaka 2002 na 2008 pia makampuni ya Microsoft na Sony yalilazimika kuchelewesha uuzaji wa michezo yao ya kompyuta kutokana na kuwa ilivunjia heshima Qur'ani Tukufu. 1116294