IQNA

Mtengeneza filamu iliyomvunjia heshima Mtume (saw) afikishwa mahakamani

17:10 - October 10, 2012
Habari ID: 2429543
Mtengenezaji wa filamu iliyomvunjia heshima Mtume Muhammad (saw) leo amefikishwa katika mahakama ya Los Angeles kwa kesi ya utapeli.
Tovuti ya Lemonde imeripoti kuwa Mark Basseley Youssef maarufu kwa jina la Nakoula Basseley Nakoula amefikishwa mahakama leo kwa mara ya pili chini ya ulinzi mkali wa polisi.
Wananchi wa Marekani wamefuatilia kesi hiyo katika ukumbi mwingine kupitia njia ya video. Baadhi ya wataalamu wanasema kuwa kuna uwezekano mkubwa kwamba mhalifu huyo atahukumiwa kifungo cha miaka miwili jela.
Nakoula Basel Nakoula ana umri wa miaka 55 na mwaka 2010 alihukumiwa kifungo miaka miwili jela kwa kupatikana na hatia ya utapeli lakini aliachiwa huru kwa masharti. Hata hivyo Disemba 23 mwaka huu jaji wa mahakama moja ya Marekani alimtambua Basseley kuwa ni mtu hatari na akaamuru atiwe mbaroni haraka iwezekanavyo.
Mmarekani huyo Myahudi ametengeneza filamu inayomvunjia heshima Mtume (saw) ya Innosence of Muslims mbayo imewakasirisha Waislamu kote duniani. Filamu hiyo imesababisha maandamano ya Waislamu na hata wasio Waislamu katika maeneo yote ya duniani. 1117386

captcha