IQNA

Mwanamke Mbosnia awa meya wa kwanza kuvaa Hijabu Ulaya

22:57 - October 10, 2012
Habari ID: 2429576
Mwanamke kutoka Bosnia amekuwa meya wa kwanza nchini Bosnia na barani Ulaya kuvaa vazi la stara la Kiislamu, Hijabu.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA barani Ulaya, Amra Babic mwenye umri wa miaka 43 alishinda katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika Oktoba 7 katika mji wa Visoko wenye wakazi 40,000 ulioko nje kidogo ya Sarajevo, mji mkuu wa Bosnia.
Babic ambaye ni mwanachama wa chama kikuu cha Bosnia cha Muslim Party of Democratic Action amesema kuwa vazi lake la Hijabu ni kigezo kwa bara la Ulaya.
Mwanasiasa huyo Mwislamu aliye na watoto watatu na ambaye pia ni mtaalamu wa masuala ya kiuchumi amesema anaamini kuwa Hijabu si kizingiti katika kazi. Ameelezea matumaini yake kuwa watu wa Ulaya wataweza kulifahamu na kuliheshimu vazi la staha la Hijabu.
Waislamu ni zaidi ya asilimia 40 ya wakazi wote milioni 3.8 nchini Bosnia.
1117401
captcha