IQNA

Wabangali walaani filamu ya Marekani inayomvunjia heshima Mtume SAW

20:49 - October 13, 2012
Habari ID: 2430751
Maelfu kwa maelfu ya Waislamu nchini Bangladesh wameendeleza maandamano ya kulaani filamu ya iliyotengenezwa Marekani inayomvunjia heshima Mtume Muhammad SAW
Katika maandamano hayo ya Jumamosi hii, Waislamu waliokuwa na hasira wamepiga nara dhidi ya Marekani na Wazayuni na kutoa wito wa kuchukuliwa hatua kali dhidi ya watengenezaji wa filamu iliyo chafu iliyobandikwa jina la kikejeli la "Innocence of Muslims". Maandamano kama hayo ya kulaani filamu hiyo yameendelea kushuhudiwa katika kila kona ya dunia. Wakati huo huo, watengenezaji filamu wawili wa Kimarekani walioshikiri kutengeneza filamu ya "Innocence of Muslims" ambayo imelipua 'ghadhabu takatifu' za Waislamu na wapenda haki kote ulimwenguni, wamezuiwa kuingia nchini Uingereza. Gazeti la Daily Telegraph linalochapishwa London limewanukuu maafisa wa Uingereza wakisema kwamba, kuingia nchini humo watengeneza filamu hao hakutakuwa na maslahi kwa wakaazi wa nchi hiyo.
1118381
captcha