Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa Muhammad Khazai amesoma taarifa ya nchi wanachama wa NAM katika kikao cha Umoja wa Mataifa kuhusu ukiukaji wa sheria unaofanywa na Israel huko Palestina.
Taarifa hiyo imesema nchi wanachama wa NAM zina wasiwasi mkubwa kuhusu hali ya mambo katika Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi wa mto Jordan.
Taarifa hiyo pia imesema NAM ina wasiwasi mkubwa kuhusu ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni unaofanywa na Israel katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina na kuongeza kuwa ujenzi huo unakiuka sheria za kimataifa.
Muhammad Khazai ambaye alikuwa akizungumza kwa niaba ya nchi wanachama wa NAM amesema jumuiya hiyo inaunga mkono matakwa ya kisheria ya wananchi wa Palestina ikiwa ni pamoja na kupewa uanachama kamili Palestina katika Umoja wa Mataifa.
kwa miaka mingi sasa wananchi wa Palestina wamekuwa wakifanya jitihada za kutambuliwa rasmi nchi yao huru katika mipaka ya mwaka 1967.