Ripoti hiyo inasema nakala hizo zilichapishwa kwa ruhusa ya al Azhar!
Gazeti hilo limeandika kuwa katika nakala hizo za Qur'ani ambazo zimechapishwa na Darul Manar ya Lebanon kunaonekana kubadilishwa na kuingiliana kwa aya za Qur'ani, suala ambalo limepotosha maana ya aya za kitabu hicho kitukufu.
Nakala hizo za Qur'ani zimechapishwa na kusambazwa chini ya usimamizi wa Idara ya Utafiti, Uandishi na Tarjumi ya Taasisi ya Uhakiki wa Kiislamu ya al Azhar tarehe 11 mwezi wa 9 mwaka 2012.
Nakala hizo za Qur'ani ziemechapishwa na kuzambazwa katika maduka ya Misri licha ya Mshauri wa Masuala ya Kisheria ya Taasisi ya Uhakiki wa Kiislamu ya al Azhar Ahmad Zaki kutangaza hapo awali kuwa kabla ya kuchapishwa nakala yoyote ya Qur'ani nakala zake mbili hukabidhiwa kwa Taasisi ya Uhakiki wa Kiislamu kwa ajili ya kupasishwa na baada ya kuthibitisha kuwa hazina makosa ya kichapa hupewa kibali cha kuchapishwa.
Hii si mara ya kwanza kuchapishwa na kusambazwa nakala za Qur'ani Tukufu zenye makosa ya kichapa nchini Misri ambazo zimeidhinishwa na al Azhar. 1121675