IQNA

Marufuku ya vazi la hijabu yafutwa Mauritius

21:13 - October 17, 2012
Habari ID: 2433653
Wizara ya Afya ya Mauritius imetangaza kuwa imefuta marufuku ya vazi la hijabu ya Kiislamu iliyokuwa imewekwa kwa wauguzi wa kike na kuongeza kuwa wauguzi hao wa kike wanaweza kwenda kazini wakiwa na vazi lao la hijabu.
Waziri wa Afya wa Mauritius alianza kushughulikia suala hilo baada ya wanafunzi wa Chuo cha Uuguzi cha Hospitali ya Victoria katika mji wa Port Louis kuwasilisha mashtaka dhidi ya wasimamizi wa chuo hicho kwa sababu ya kuzuia vazi la hijabu.
Waziri wa Afya wa Mauritius amesema kuwa tatizo la wanafunzi wa chuo cha wauguzi limetatuliwa na tangu sasa wanaweza kwenda kazini wakiwa na vazi la hijabu.
Ameongeza kuwa hakuna sheria yoyote inayopiga marufuku vazi la hijabu katika maeneo ya kazi.
Waziri wa Kazi wa Mauritius pia amekosoa hatua za kuzuia vazi la hijabu mahospitalini na katika vituo vya umma na ametaka sheria zote kuhusu suala hilo zitazamwe upya. 1121617


captcha