IQNA

Ombi la mcheza filamu inayovunjia heshima Uislamu lakataiwa tena

19:55 - October 20, 2012
Habari ID: 2434823
Mahakama ya Federali ya Marekani imekataa tena ombi mcheza filamu iliyomvunjia heshima Mtume (saw) aliyeitaka YouTube kuondoa sehemu aliyocheza yeye katika filamu ya Innocence of Muslims.
Uamuzi huo wa Mahakama ya Federali wa Marekani ulitangazwa jana baada ya mchezaji huyo wa filamu chafu kuitaka YouTube iondoe vipengee alivyocheza yeye katika filamu hiyo.
Cindy Lee Garcia amedai kuwa hakujua nini kinachozungumziwa katika filamu hiyo. Amesema kuwa alicheza katika filamu nyingine ndefu iliyopewa jina na Wapiganaji wa Jangwani na kwamba filamu hiyo ilibadilishwa jina la kupewa jina jingine la Innocence of Muslims isiyoyokuwa na uhusiano kabisa na ile ya asili.
Lee Garcia alikuwa mtu wa kwanza kufungua mashtaka dhidi ya YouTube baad aya maandamano makubwa ya Waislamu duniani kote dhidi ya filamu hiyo. Anasema anaunga mkono uhuru wa kusema lakini haafikiani na kazi za watengeza filamu za kuvunjia heshima matukufu ya kidini.
Hatua ya mtandao wa YouTube ya kurusha hewani filamu ya Innocence of Muslims inayomvunjia hesma Mtume Muhammad (saw) imepingwa vikali na Waislamu kote duniani. 1122999
captcha