IQNA

Darul Qur’an ya Gaza yapata uanachama katika Jumuiya ya Kimataifa ya Qur’ani

21:56 - October 22, 2012
Habari ID: 2436205
Jumuiya ya Qur’ani na Suna za Mtume ya Gaza imepata uanachama katika Jumuiya ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur’ani Tukufu.
Mkurugenzi Mkuu wa Darul Qur’ani ya Gaza Mahmoud al Khas amesema kuwa jumuiya hiyo imepata uanachama katika Jumuiya ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur’ani kutokana na jitihada kubwa za viongozi na wafanyakazi wake.
Uanachama huo utaiwezesha jumuiya ya Darul Qur’an kupata misaada na kuimarisha shughuli zake za kutoa elimu na mafunzo ya Qur’ani na Suna za Mtume. 1123315


captcha