Sinad Hadzic mwenye umri wa miaka 47 ambaye amevuka nchi sita akitembea kwa miguu amesema baada ya kuwasili katika mji mtakatifu wa Makka kwamba, alikuwa na matarajio ya kwenda kuhiji Makka siku nyingi lakini hakuwa na masurufu ya safari na kwa msingi huo aliamua kutembea kwa miguu kueleka Makka.
Hadzic amewasili Makka baada ya kukata masafa ya kilomita 5900 kutoka kijijini kwake huko Bosnia.
Muislamu huyo ambaye alikuwa akitembea baina ya kilomita 20 hadi 30 kwa siku, amepita katika nchi sita zikiwemo Uturuki, Jordan na Syria.
Mwslamu huyo wa Bosnia alibeba nakala moja ya Qur’ani Tukufu, Injili, ramani ya nchi alikopitia na fedha kidogo alizokuwa nazo na katika kipindi chote cha safari alilala misikitini, kwenye madrasa na mahala alipotayarishiwa na watu wema waliomsaidia.
Sinad Hadzic ameungana na mamilioni ya Waislamu walioko Makka kwa ajili ya kutekeleza ibada ya hija. 1124471