IQNA

Ayatullah Kashani:

Waislamu kote duniani wanapaswa kushikamana

23:44 - October 26, 2012
Habari ID: 2437961
Khatibu wa swala ya Idul Adh'ha iliyoswaliwa leo hapa mjini Tehran amewapongeza Waislamu wote kwa sikukuu hii kubwa na kuwataka washikane na Watu wa Nyumba ya Mtume Muhammad (saw).
Ayatullah Imami Kashani amesema katika hotuba za swala ya Idi kwamba umoja na mshikamano katika umma wa Kiislamu kote dunia hususan katika zama hizi ambapo maadui wanataka kuwadunisha kwa kuvunjia heshima matukufu yao kama kutengeneza filamu zinazomdhalilisha Mtume Muhammad (saw), ni jambo la lazima.
Imamu wa swala ya Idi mjini Tehran ametilia mkazo umoja wa Kiislamu na udharura wa kusimama kidete mbele ya vitisho vinavyoukabili ulimwengu wa Kiislamu.
Vilevile ameashiria uwezo mkubwa wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika mfumo wa kimataifa na kuwausia wananchi wa Iran kulinda heshima na fahari hiyo iliyopatikana kutokana na damu ya mashahidi na kushirikiana katika kupamba na matatizo yanayosababishwa na vikwazo vya nchi za Magharibi. 1126284
captcha