Mshauri wa ngazi za juu wa Rais wa Marekani Barack Obama katika masuala ya kupambana na ugaidi John O. Brennan, ametangaza kuwa, Washington inaushinikiza Umoja wa Ulaya (EU) ili uiweke harakati ya Hizbullah ya Lebanon katika orodha ya makundi ya kigaidi duniani.
Akiukosoa Umoja wa Ulaya kwa kuiondoa harakati hiyo ya muqawama kwenye orodha hiyo, Brennan amesema, nchi za Ulaya pia zinatakiwa kuchukua hatua kama iliyochukuliwa na Marekani ya kuiweka Harakati ya Hizbullah katika orodha ya makundi ya kigaidi duniani.
Tarehe 24 Julai mwaka huu na licha ya mashinikizo ya Washington na utawala haramu wa Kizayuni wa kutaka kuiweka harakati hiyo katika orodha ya makundi ya kigaidi, Umoja wa Ulaya uliiondoa harakati hiyo ya Hizbullah katika orodha hiyo.
EU pia ilisema kuwa, unaitambua Hizbullah kuwa ni chama cha kisiasa kinachoendesha shughuli zake nchini Lebanon kwa njia za kisheria na kwamba, viongozi wa Ulaya hawaoni sababu ya kuiweka harakati hiyo katika orodha ya ugaidi. 1127285