IQNA

Tamasha ya Qur'ani na Ahlul Bait yaanza leo Tehran

17:24 - October 30, 2012
Habari ID: 2440718
Sherehe ya Tamasha ya 27 ya kimataifa ya Qur'ani na Ahlul Bait ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Iran imeanza leo ikihudhuriwa na Waziri wa Utamaduni na viongozi wengine wa ngazi za juu hapa nchini.
Mkuu wa Jumuiya ya Basij ya Wanafunzi wa vyuo vikuu hapa nchini Hussein Fadai ambaye alikuwa wa kwanza kuzungumza katika tamasha hiyo amewakaribisha wageni waalikwa na kusema kuwa Qur'ani ukufu ndio johari inayohitajiwa na wanadamu wa dunia ya leo na kwamba mabeberu kote duniani wanafanya njama za kuwazuia watu wasisikilize sauti ya kitabu hicho kitakatifu.
Amesema ana matumaini kwamba tamasha hiyo itafungua mlango wa kutadabari, kutafakari na kuhifadhi kitabu kitukufu cha Mwenyezi Mungu.
Baadaye Waziri wa Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu wa Iran Sayyid Muhammad Husseini alihutubia kikao cha ufunguzi. Amesema kuwa heshima na nguvu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inatokana na kufuata mafundisho ya Qur'ani na Ahlul Bait wa Mtume (saw) na jambo hilo linawakasirisha mabeberu na tawala za kidhalimu ambazo sasa zimeamua kulipiza kisasi kwa kuchoma moto Qur'ani Tukufu na kutengeneza filamu zinazomvunjia heshima Mtume Muhamamd (saw).
Sayyid Hussein amesema wakoloni hao wa Magharibi wana woga wa kutekelezwa mafundisho ya Qur'ani ambayo yanapinga satuwa na ushawishi wa mabeberu katika ulimwengu wa Kiislamu. Waziri wa Utamaduni wa Iran amesema kuwepo Qur'ani tu bila ya kutekelezwa mafundisho yake hakuwatii hofu mabeberu na mfano wa wazi wa jambo hilo ni kuwepo maelfu ya makarii wa Qur'ani huko Misri katika kipindi cha utawala wa dikteta Hosni Mubarak suala ambalo halikuizuia nchi hiyo kuwa na uhusiano na ushirikiano mkubwa na tawala za kibeberu na kidhalimu. 1129100
captcha