Amnesty International imetoa tuhuma hizo kutokana na mwenendo wa serikali ya Addis Ababa wa kuwalenga na kuwatia nguvuni Waislamu kwa kosa eti la kushiriki kwenye maandamano ya amani ya kudai uhuru wa kidini.
Ripoti ya Amnesty International imesema kuwa, serikali ya Ethiopia imekuwa ikiwakandamiza Waislamu na kuwatuhumu kuwa wanaendesha harakati za kigaidi kwa sababu tu ya kushiriki kwenye maandamano ya amani. Imesema mwenendo wa serikali ya Ethiopia na Waislamu wanaoandamana kudai uhuru wa kidini unakiuka sheria za haki za binadamu.
Imesema kuwa serikali ya Addis Ababa imekataa kushughulikia dhulma wanazofanyiwa Waislamu wala kufanya mazungumzo nao na badala yake imekuwa ikitumia mabavu kukandamiza maandamano yao.
Waislamu nchini Ethiopia wamekuwa wakiandamana wakipinga uingiliaji wa serikali ya nchi hiyo katika masuala yao ya kidini.
Inakadiriwa kuwa Waislamu wa Ethiopia wanaunda aseilimia 50 ya jamii yote ya nchi hiyo. 1132389