IQNA

Maulamaa wa Najaf wako tayari kuzungumza na wenzao wa al Azhar

19:33 - November 10, 2012
Habari ID: 2445760
Imamu wa Swala ya Ijumaa katika mji mtakatifu wa Najaf nchini Iraq ametangaza kuwa maulamaa wa mji huo wako tayari kukutana na kufanya mjadala na wenzao wa al Azhar nchini Misri.
Sayyid Sadruddin Qubanchi ameyasema hayo kufuatia vikao vinavyofanyika katika al Azhar dhidi ya madhehebu ya Waislamu wa Shia nchini Misri.
Amesema kuwa Najaf iko tayari kwa ajili ya kukabiliana kifikra na harakati zinazopiga vita madhehebu ya Kiislamu ya Shia zinazofanyika katika kalibu ya vikao vinavyohudhuriwa na Mufti wa Misri Sheikh Ali Gumaa na maulamaa wengine wa al Azhar ili kuzuia satua na kuenea zaidi madhehebu ya Kiislamu ya Shia nchini Misri.
Sayyid al Qubanchi amesema inatarajiwa kuwa al Azhar na maulamaa wake watawaelimisha wananchi wa Misri kuhusu madhehebu ya wafuasi wa Ahlul Bait wa Mtume (saw) na itikadi na imani zao.
Al Azhar ya Misri imeonesha kuathiriwa na makundi ya ya kisalafi na yale yanayowakufurisha Waislamu kwa kuruhusu vikao vya makundi hayo kufanyika ndani ya chuo hicho kikubwa zaidi cha taaluma za Kiislamu cha madhehebu ya Suni. Vikao hivyo vinahujumu Waislamu wa madhehebu ya Shia. 1134731
captcha