IQNA

UN: Nchi jirani na Myanmar ziwapokee wakimbizi wa Kiislamu

11:47 - November 15, 2012
Habari ID: 2448777
Kamisheni Kuu ya Wakimbizi ya Umoja wa Mataifa imezitaka nchi jirani na Myanmar kufungua mipaka yao mbele ya Waislamu wanaokimbia mauaji na ukatili nchini kwao huko Myanmar.
Wito huo wa UNHCR umetolewa kutokana na wasiwasi juu ya hatima isiyojulikana ya boti kadhaa zilizojaa Waislamu wa kabila la Rohingya zilizosimamishwa karibu na mpaka wa Myanmar na Bangladesh.
Wakati huo huo Umoja wa Mataifa umeitaka serikali ya Myanmar kusitisha mara moja machafuko nchini humo.
Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameeleza kutiwa wasiwasi na kuendelea machafuko huko Myanmar na kuitaka serikali ya nchi hiyo kukomesha haraka iwezekanavyo mashambulizi dhidi ya Waislamu wa nchi hiyo. Martin Nisirky msemaji wa Ban Ki Moon Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameashiria hali ngumu inayowakabili wakimbizi wa Kiislamu wa Myanmar na kueleza kuwa Umoja wa Mataifa unaitaka serikali ya nchi hiyo kusitisha mara moja mashambulizi dhidi ya Waislamu na kuzingatia hali ya Waislamu wa nchi hiyo.
Nisirky amesema hali ni ya kutia wasiwasi huko katika mkoa wa Rakhine na maelfu ya watu wameamua kuukimbia mkoa huo kupitia njia ya majini na kwamba wamepata ripoti mbaya kuhusu hali za watu hao. 1137462
captcha