IQNA

Israel yatekeleza jinai Ukanda wa Gaza, mashahidi waongezeka

13:48 - November 15, 2012
Habari ID: 2448833
Vikosi vya jeshi la Israel limefanya mashambulizi mapya ya anga kaskazini mwa Ukanda wa Gaza, huku utawala huo haramu ukisema kwamba utazidisha mashambulizi hayo.
Mashambulizi hayo ya Israel yalianza Jumatano jioni kwa kumuua shahidi Ahmed al Jabari, aliyekuwa kamanda wa Brigedi ya Izzuddin Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu Palestina hamas huko Gaza.

Mashambulizi hayo ya anga ya utawala ghasibu wa Israel pia yamewaua shahidi raia wengine 10 wa Kipalestina. Wazayuni ambao wanahofia mashambulizi ya makombora ya wanaharakati wa Palestina wameliweka jeshi lao tayari na kutangaza kwamba watafanya mashambulizi ya nchi kavu iwapo italazimu.

Wakati huo huo Mamalaka ya Ndani ya Palestina imelitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liichukulie hatua Israel, ambayo imeanza mashambulizi mapya dhidi ya Ukanda wa Gaza. Riyadh Mansour Mwakilishi wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina katika UN amesema, mashambulizi hayo ya Israel ni jinai dhidi ya binadamu na kwamba Tel Aviv inapaswa kusitisha hujuma zake hizo dhidi ya wananchi wa Palestina ambao inakalia kwa mabavu nchi yao, inawazingira na kuwaua ovyo.
captcha