IQNA

Sayyid Nasrallah:'Kutuma silaha Ghaza ndio wajibu mkubwa zaidi'

9:57 - November 20, 2012
Habari ID: 2451564
Katibu Mkuu wa chama cha Hizbullah cha Lebanon amesema kuwa kuwapelekea silaha wanamapambano wa Palestina huko Ghaza ni katika mambo ya wajibu zaidi hivi sasa.
Katibu Mkuu wa chama cha Hizbullah cha Lebanon amesema kuwa kuwapelekea silaha wanamapambano wa Palestina huko Ghaza ni katika mambo ya wajibu zaidi hivi sasa. Sayyid Hasan Nasrullah alisema hayo jana usiku kwa mnasaba wa mwezi wa Muharram na huku akizilaumu tawala wa nchi za Kiarabu kwa kutochukua hatua za maana za kukomesha mashambulizi ya kikatili ya Wazayuni huko Ghaza amesema kuwa, inashangaza kuona kuwa baadhi ya tawala za nchi za Kiarabu zinatuma meli za silaha kwa waasi wa Syria lakini hazithubutu kutuma hata risasi moja kwa wananchi wa Ghaza wanaokabiliwa na ukatili mkubwa kutoka kwa Wazayuni maghasibu. Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon ameongeza kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel utakuwa unajidanganya sana utakapodhani kuwa makombora ya wanamuqawama huko Palestina yameisha na amezitaka nchi za Kiarabu zinazopakana na Palestina zifungue mipaka yao kwa ajili ya kutumwa silaha zaidi kwa Wapalestina wanaojilinda mbele ya ukatili wa Wazayuni. Aidha amesema hadi hivi sasa wananchi wa Ghaza wamefanikiwa kusimama imara na kishujaa mbele ya mashambulizi ya kikatili ya Wazayuni. Wapalestina wamesema watakubaliana na usimamishaji vita pale tu Israel itakapoacha kuwashambulia kiholela Wapalestina na kufunguliwa mipaka ya Ghaza.
1140810
captcha