Mashindano hayo yatasimamiwa na Wizara ya Wakfu ya Libya na kuwashirikisha wawakilishi kutoka nchi mbalimbali za Kiislamu.
Mkuu wa Idara ya Mashindano ya Qur'ani na Suna za Mtume ya Libya Muhammad al Rabu amesema kuwa kamati ya mashindano hayo imewaalika makari wa Qur'ani Tukufu kutoka nchi 120 za Kiislamu kwa ajili ya kushiriki katika mashindano hayo ya kimataifa na kwamba hadi sasa nchi 53 zimethibitisha kwamba zitashiriki.
Ameongeza kuwa kamati ya majaji wa mashindano hayo itaongozwa na Sheikh Aiman Rushdi Suwaid kutoka Syria na inajumuisha majaji hodari kutoka nchi za Syria, Uturuki, Tunisia, Burkina Faso na Libya.
Al Rabu amesema washiriki katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Libya wanapaswa kuwa raia wa nchi wanazowakilisha na wawe na umri wa zaidi ya miaka 25.
Amesema mshindi wa kwanza wa mashindano hayo atapewa zawadi ya dinari laki moja za Libya, wa pili elfu 80, wa tatu elfu 60, wanne elfu 40 na wa tano elfu 20. 1142330