Mashindano hayo ambayo yamepewa jina la Mashindano ya Mfalme Abdul Aziz yanasimamiwa na Wizara ya Wakfu ya Saudia yakiwashirikisha makarii 164 kutoka nchi 53.
Viongozi wa Saudi Arabia hawakuwaalika makarii wa Qur'ani kutoka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa mwaka wa pili mfululizo.
Viongozi wa Jumuiya ya Wakfu ya Iran wanasema kutoalikwa wasomaji Qur'ani wa Iran kunatokana na ama masuala ya kisiasa au uwezo mkubwa wa makarii wa Jamhuri ya Kiislamu, kwani maafisa wa Saudia hawataki kuona Wairani wakishinda mashindano hayo. 1146279