IQNA

UN yapinga ujenzi wsa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi Palestina

12:55 - December 03, 2012
Habari ID: 2457796
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amekosoa mpango wa utawala wa Kizayuni wa Israel wa kupanua vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.
Ban Ki-Moon ameeleza wasi wasi wake mkubwa kuhusiana na mpango wa Israel wa kupanua mamia ya vitongoji katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu. Utawala wa Kizayuni wa Israel hivi karibuni ulipasisha mpango mpya wa kujenga nyumba nyingine 3000 katika ardhi za Quds Mashariki na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
Hayo yanajiri katika hali ambayo, Catherine Ashton Mkuu wa Siasa za Kigeni wa Umoja wa Ulaya amesema kuwa uendelezaji wa ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Palestina unakinzana na sheria za kimataifa na ameutaka utawala wa Kizayuni wa Israel uheshimu kikamilifu ahadi zake za kuanzishwa tena mazungumzo ya amani kati ya Wazayuni na Wapalestina. 1147410
captcha